KUTEKWA
NYARA!!
“Nilikamatwa na kuteswa na polisi wa Misri kwa kuhoji imani
yangu katika Uislamu” Na Mark Gabriel
Ilikuwa saa 9 kamili alfajiri wakati baba yangu aliposikia mlango wa nyumba yetu
ukigongwa. Wakati alipofungua mlango, watu 15 hadi 20 waliingia kwa haraka ndani
wakiwa wamebeba silaha za Urusi Kalashnikov za uvamizi. Walikimbilia ghorofani
wakipitapita kila mahali katika nyumba wakiwaamsha watu na kunitafuta mimi.
Walikuwa wametapakaa kila mahali mle ndani kabla mmoja wao hajanikuta nimelala
kitandani mwangu. Wazazi wangu, kaka zangu na wenzi wao na watoto walikuwa
wameamka, wakilia na kuhofia sana wakati hao watu waliponiburuza na kuondoka
na mimi. Kila mtu wa eneo lile alisikia habari za vurumai hizo. Nilipelekwa mahali
palipoonekana kama jela na nikawekwa rumande. Asubuhi yake wazazi wangu kwa
hasira na majonzi walijaribu kutafuta kwamba nini kilichonitokea. Moja kwa moja
walienda kituo cha polisi na kudai “mtoto wetu yuko wapi? Lakini hakuna yeyote
aliyejua lolote juu yangu. Nilikuwa katika mikono ya polisi wa siri wa Misri.
Matukio Yaliyosababisha Kukamatwa Kwangu
Miaka kumi na tano iliyopita nilikuwa Imamu wa msikiti katika jiji la Giza, Misri,
mahali ambapo yale mapiramidi maarufu ya Misri yamepangwa. (Imam wa msikiti ni
wadhifa unaofanana na mchungaji wa kanisa la Kikristo) Nilihubiri ujumbe wa wiki
siku za ijumaa kuanzia saa 6 hadi 7 mchana, ikiwa ni pamoja na kufanya wajibu
zinginezo zilizonihusu.
Ijumaa moja ujumbe wangu wa wiki ulikuwa Jihad. Niliwaambia watu 250
waliokuwa wamekaa uwanjani mbele yangu Jihad katika uislamu inatetea taifa la
Kiislam na Uislam dhidi ya mashambulizi ya maadui. Uislam ni dini ya amani na
itapigana na yule anayepigana nayo tu. Hawa makafiri, wamataifa, wapotoshaji,
Wakristo na wanaomhuzunisha Allah, Wayahudi, mbali ya wivu wa Uislam wa amani
na Mtume wake; walieneza uongo kwamba Uislam ulienezwa kwa upanga na kwa
nguvu kali sana zenye vurugu. Makafiri na washitaki wa Uislam hawayakubali
maneno ya Allah.
Katika hatua hii nilinukuu kutoka katika Koran “wala usimuue yeyote ambaye
uuaji kwa Allah umekatazwa ila kwa sababu ya haki” (Surah 17:33 Koran Tukufu).
Nilipozungumza maneno haya ndio kwanza nilikuwa nimetoka kuhitimu Chuo Kikuu
cha Al-Azhar cha Kairo Misri. Chuo Kikuu cha zamani na chenye fahari zaidi cha
Kiislam duniani. Kinafanya kazi kama mamlaka ya kiroho ulimwenguni mwote.
Nilikuwa nafundisha katika Chuo Kikuu na nilikuwa Imam siku za mwisho wa juma
katika msikiti huu. Nilikuwa nakihubiri kile walichonifundisha, lakini kwa ndani nilihitaji
kuyaweka mawazo yangu kwenye nafsi yangu. Hata hivyo, nilijua kile
kinachowapata watu waliohitilafiana na agenda za Al-Azhar. Watafukuzwa na
wasingeruhusiwa kufundisha Chuo Kikuu kingine chochote katika Taifa hilo.
Nilifahamu kwamba nilichokuwa nakifundisha pale msikitini na katika Al-Azhar
hakikuwa kile nilichokiona katika Koran, ambayo nilikuwa nimeikariri yote nikiwa na
umri wa miaka 12. Kilichonichanganya zaidi ni kwamba niliambiwa nihubiri kuhusu
Uislam wa upendo, wema na msamaha. Wakati huo huo wale waumini
wakereketwa; wale ambao ndio waliotarajiwa kuishi kwa kutenda Uislam kamili;
walikuwa wakiyapiga mabomu Makanisa na kuua Wakristo. Kwa wakati huohuo
vuguvugu la jihad lilikuwa limepamba moto ndani ya Misri. Matukio ya mashambulizi
na kupigwa mabomu, dhidi ya Wakristo yalikuwa ya kawaida sana. Ilikuwa ni
sehemu ya maisha ya kila siku.
Kuutafuta Ukweli
Wakati mwingi nilijaribu kutazama kimantiki aina ya Uislam niliokuwa naufanya
kwa kujiambia nafsi yangu “Sawa, hauko mbali sana na ukweli. Kwanza kuna mstari
katika Koran kuhusu upendo, amani, msamaha na huruma. Unachotakiwa tu ni
kutojali kipengele kinachohusu jihad na cha kuua wasiokuwa Waislam.” Nilipitia kila
tafsiri ya koran nikijaribu kukwepa Jihad na kuua wasio Waislamu, bado niliendelea
kugundua utekelezaji wa hayo ukiungwa mkono. Wanazuoni walikubali kwamba
Waislam lazima wakazie Jihad kwa makafiri (wale wanaoukataa Uislam na waasi
wale wanaoucha Uislam). Bado Jihad haikuwa na maelewano na mistari
iliyozungumzia kuishi kwa amani na wengine. Mikanganyo yote katika Koran ilikuwa
kweli inasababisha matatizo kwa imani yangu. Nilitumia miaka 4 kusomea Digrii
yangu ya kwanza, nilihitimu nikiwa wa pili kati ya wanafunzi elfu sita. Halafu kulikuwa
na miaka mingine 4 kwa ajili ya Digrii yangu ya pili na mitatu zaidi kwa ajili ya Ph.D
(udaktari wa falsafa) yote nikisomea Uislam.
Ninafahamu mafundisho vizuri katika sehemu moja pombe imekatazwa; katika
sehemu nyingine imeruhusiwa (linganisha Surah 5:90-91 na Surah 47:15). Katika
sehemu moja Koran inasema Wakristo ni watu wema ambao wanampenda na
kumwabudu Mungu mmoja, kwahiyo mnaweza kuwa marafiki nao (Surah
2:62,3:113-114). Halafu unakuta mstari mwingine unaosema Wakristo lazima
waslim, walipe kodi la sivyo wauwawe kwa upanga (Surah 9:29) Wanazuoni
wanasuluhisho la kitheolojia kwa matatizo haya, lakini nashangaa ni jinsi gani Allah,
mwenye enzi na mwenye nguvu sana, awe aidha amejichanganya mwenyewe
namna hii kubwa au anabadili nia yake kwa kiasi kikubwa namna hii, hata nabii wa
Kiislam Mohammed, aliitekeleza imani yake katika njia ambazo zinapingana na
Koran. Koran inasema Mohammed alitumwa ili kuonyesha rehema za Mungu kwa
ulimwengu. Lakini alikuja kuwa dikteta wa kivita, akishambulia, kuua na kuchukua
mali na kupora ili kufadhili himaya yake. Iweje hivyo iwe ni kuonyesha rehema?
Allah, Mungu aliyefunuliwa katika Koran, sio Baba wa Upendo. Inasema kwamba
anatamani kuwaongoza watu upotevuni (Surah 6:39,126). Hawasaidii wale
walioongozwa nae upotevuni (Surah 30:29) na anatamani kuwatumia kujaza watu
kuzimu (Surah 32:13). Uislamu umejaa ubaguzi dhidi ya wanawake, dhidi ya wasio
Waislam, dhidi ya Wakristo na zaidi hasahasa dhidi ya Wayahudi.
Chuki imejengwa katika dini. Historia ya Uislam ambayo ilikuwa ndio eneo langu
nililobobea hasa, ingeweza ikaainishwa kama mto wa damu. Mwishoni nilifikia
mahali ambapo nilikuwa nahoji imani na Koran pamoja na wanafunzi wangu katika
Chuo Kikuu. Baadhi yao walikuwa wanachama wa vuguvugu la ugaidi na
walighadhibika. “Huwezi kuushutumu Uislam. Ninini kimetokea? Unatakiwa
utufundishe. Unatakiwa kukubaliana na Uislam”. Chuo Kikuu kikasikia kuhusu hilo,
na niliitwa kwa ajili ya mkutano Desemba 1991. Kufupisha mkutano, nikawaambia
kilichokuwepo moyoni mwangu. Siwezi tena kusema kwamba Koran imekuja moja
kwa moja toka mbinguni au toka kwa Allah. Huu hauwezi kuwa ufunuo wa Mungu wa
kweli. Haya yalikuwa maneno ya kufuru kubwa katika mtazamo wao. Wakanitemea
mate usoni, mtu mmoja akanitukana “wewe mkufuru! mbegu haramu!” Chuo Kikuu
kikanifukuza na kuita kikosi cha polisi wa siri wa Misri.
Gereza la Misri
Kutumia muda pamoja na polisi wa siri wa Kimisri ni tofauti sana na kutembelea
gereza la Marekani. Kwa siku tatu sikupewa chakula wala maji. Katika siku ya nne,
mahojiano yakaanza. Aliyekuwa akiniuliza maswali alikaa nyuma ya meza nami
nimekaa upande wa pili. Nyuma yangu walikuwepo maofisa wa polisi wawili au
watatu. Walikuwa na uhakika kuwa nilikuwa nimehubiriwa injili na kubadlilika kuwa
Mkristo, kwa hiyo mhojaji akakazania kunisumbua.. “Ni mchungaji gani
uliyezungumza naye? Umekuwa ukitembelea kanisa gani? Kwanini umeukana
Uislam?”
Aliniuliza maswali mengi. Safari moja nilisita kwa muda mrefu hadi nilipojibu.
Aliwaashiria wanaume waliokuwa nyuma yangu. Waliukunja mkono wangu na
kuushikilia chini ya dawati. Aliyekuwa akiniuliza maswali alishikilia sigara
iliyowashwa. Alinikaribia na kuizimia juu ya mkono wangu. Bado kovu lile ninalo hadi
leo. Pia ninalo kovu kwenye mdomo wangu mahali alipopafanyia jambo hilohilo.
Mara nyingine alitumia sigara pale alipokasirika na mara nyingine maofisa
walinipiga usoni. Jinsi aliyekuwa akinihoji alivyoendelea, hasira na shinikizo ndivyo
zilivyoongezeka kuwa kubwa kwake. Mara moja walileta mbanio wa mkaa mle
chumbani. Nilishangaa hili ni la nini? Kisha aliyekuwa ananihoji alitaka kuzungumzia
suala lake, niligundua kilichokuwa kikiendelea. Ule mbanio ulichomwa ukawa
mwekundu sana na ofisa mmoja aliukandamiza kwenye nyama za mkono wangu wa
kushoto.
Walinitaka nikiri kwamba nimebadili dini lakini nikawaambia, “sijaukana Uislam,
nilikisema tu kile ninachoamini. Mimi ni mtu wa taaluma, mimi ni mtu ninayefikiri.
Nina haki ya kujadili somo lolote la Uislam. Hii ni sehemu ya kazi yangu na sehemu
ya maisha yangu ya kitaaluma. Nisingeweza hata kuota ndoto za kubadilika kutoka
katika Uislam. Ni damu yangu, desturi yangu, lugha yangu, familia yangu na maisha
yangu. Lakini kama mkinishutumu kwa kubadilika kutoka katika Uislam kwa yale
ninayowaambieni,basi niondoeni kwenye Uislam. Sitajali kuwa nje ya Uislam.”
Mbwa
Baadae maofisa walinichukua hadi kwenye mlango wa chumba kidogo na
kusema “kuna mtu akupendae sana ambaye anataka kukutana na wewe”. Nikauliza,
“ni nani?” Nilitumaini alikuwa mmoja wapo wa watu wa familia yangu au rafiki
aliyenitembelea au kunitoa nje ya gereza. Wakasema, “Humfahamu lakini yeye
anakujua” Walifungua mlango wa chumba na ndani nikaona mbwa mkubwa.
Hapakuwapo na kitu kingine chochote mle chumbani. Watu wawili waliniingiza
mle chumbani na wakaniacha humo na kufunga mlango. Hii ilikuwa mara yangu ya
kwanza moyo wangu kulia kwa nguvu. Moyoni mwangu nilimlilia Muumba wangu;
“Wewe ni Baba yangu, Mungu wangu, wewe ndie utakae nitunza. Unawezaje
kuniacha katika mikono hii miovu? Sifahamu kile wanachojaribu kunitendea, lakini
nafahamu utakuwa pamoja nami na siku moja nitakuona Wewe na kukutana na
Wewe”. Nilitembea hadi katikati ya chumba kile kitupu na nikaketi chini kwenye
sakafu nikiwa nimepishanisha miguu yangu mtindo wa x. Mbwa alikuja na kuketi
chini mbele yangu. Dakika zilipita huyu mbwa akiwa amenitazama kwa makini.
Nilimwangalia macho yake yakiwa yananitazama kuanzia juu hadi chini tena na
tena. Niliomba ndani ya moyo wangu kwa Mungu ambaye nilikuwa simfahamu bado.
Yule mbwa akasimama na akaanza kutembea kwenye duara kunizunguka mimi,
kama vile mnyama aliye tayari kula kitu fulani. Kisha akaja upande wangu wa kulia
na kulamba sikio langu kwa ulimi wake. Nilikuwa nimechanganyikiwa sana. Alikaa
pale, na nililala usingizi. Nilipokuja kuamka yule mbwa alikuwa kwenye kona ya kile
chumba. Alinikimbilia, kama vile kusema habari ya asubuhi. Kisha akalamba sikio
langu la kulia tena na akakaa upande wangu wa kulia.
Wakati maofisa walipofungua mlango waliniona nikiomba na mbwa akiwa kaketi
pembeni yangu. Nilimsikia mmoja wao akisema “Siwezi kuamini kuwa huyu mtu ni
mwanadamu. Huyu mtu ni ibilisi ni Shetani”. Katika hatua hii hata mimi sikufikiri
kwamba aliyekuwa akinihoji ni mwanadamu. Nilikuwa nimewekwa ndani kwa kule tu
kuuhoji Uislam, sasa imani yangu ilikuwa kweli imetikiswa. Muda huu wote familia
yangu ilikuwa ikijaribu kutafuta pale nilipokuwa. Hawakufanikiwa hadi pale mjomba
wangu, ambaye alikuwa na cheo kikubwa katika bunge la Misri aliporudi nyumbani.
Mama yangu alimwita akilia kwa huzuni, “Kwa wiki mbili hatujui alipo mwenetu,
amekwenda”. Mjomba wangu alikuwa na mawasiliano yaliyokuwa yakihitajika. Siku
kumi na tano baada ya kutekwa kwangu nyara alikuja gerezani na kunipeleka
nyumbani.
Mwaka Mmoja Bila Imani
Kwa mwaka mmoja niliishi bila imani. Sikuwa na Mungu wa kumuomba, wa
kumuita au kumwishia. Niliamini katika uwepo wa Mungu ambaye alikuwa mwenye
rehema na haki, lakini sikuweza kufahamu Mungu wa jinsi hiyo ni nani. Je, alikuwa ni
mungu wa Waislam, wa Wakristo au Wayahudi au alikuwa mnyama; kama vile
ng’ombe wa Kihindu? Sikuwa na maarifa ya jinsi ya kumtafuta.
Unatakiwa kufahamu kwamba kama Mwislam akifikia hitimisho kwamba Uislam
sio wa kweli na akiwa hana dini ya kugeukia, atakuwa na wakati mgumu sana katika
maisha yake. Imani iko katika kiini cha maisha ya mtu wa Mashariki ya Kati.
Hawezi kufikiria namna ya kuishi bila kumjua Mungu wake. Kwa kipindi chote hiki
cha mwaka mmoja, mwili wangu ulidhihirisha maumivu ambayo yalikuwa kwenye
roho yangu. Ijapokuwa nilikuwa na mali za aina zote nilizohitaji, nilipata pigo la
uchovu wa ndani sana kwa kule kujaribu mfululizo kutumia ufahamu wangu kupata
picha ya Mungu wa kweli anavyofanana.
Nilikuwa naumwa na kichwa mfululizo . Nilikwenda kwa daktari ambaye alikuwa
ni ndugu wa familia yetu. Akafanyia uchunguzi kichwa changu kwa (kipimo cha scan)
lakini hakuona tatizo lolote. Aliniandikia dawa zitakazonisaidia.
Hotuba Ya Mlimani
Niliishia kulitembelea duka la dawa lililokuwa karibu kila wiki mara mbili ili kupata
paketi ya vidonge. Nilikuwa nachukua kidogo kidogo nikitarajia maumivu ya kichwa
yangeondoka moja kwa moja. Baada ya kwenda pale dukani kwa kitambo yule
mfamasia akaniuliza, “Ni nini kinachoendelea kwenye maisha yako?” Nikamjibu,
“Sina tatizo lingine ila jambo moja tu. Ninaishi bila Mungu sifahamu Mungu ni nani”
Akaniambia, “Lakini wewe ulikuwa Profesa katika Chuo Kikuu kinachoheshimika
zaidi nchini Misri. Familia yako inaheshimika sana katika jumuiya hii” “Hiyo ni kweli”
Nilijibu, ‘lakini nimegundua upotofu mwingi katika mafundisho yao. Siamini tena
kama nyumba yangu na familia yangu wamejengwa katika misingi ya ukweli.
Nimekuwa nikijifunika siku zote katika uongo wa Kiislamu, sasa najiona niko uchi.
Nawezaje kuujaza utupu ulioko moyoni mwangu? Tafadhali nisaidie’ “Sawa”
Alisema, “Leo nitakupa vidonge hivi na nitakupatia kitabu hiki-Biblia”
Nilikichukua kile kitabu nyumbani na kukifungua bila mpangilio maalum. Macho
yangu yakaangukia Matayo 5:38 “Mmesikia kwamba imenenwa, jicho kwa jicho na
jino kwa jino; Lakini mimi nawaambia, msishindane na mtu mwovu; lakini mtu
akupigaye shavu la kuume mgeuzie na la pili.” Mwili wangu wote ukaanza
kutetemeka. Nilikuwa nimesoma Koran na maneno maisha yangu yote hata mara
moja sikukutana na maneno yenye uvuvio kama haya. Nilikutana uso kwa uso na
Bwana Yesu Kristo, nikapoteza muda mwingi bila kufanya chochote.
Ilionekana kana kwamba nilikuwa nimeketi juu ya mawingu juu ya kilima; na
mbele yangu alikuwepo mwalimu mkuu kuliko wote ulimwenguni akiniambia habari
za siri za mbinguni na moyo wa Mungu. Ningeweza kulinganisha kwa urahisi Biblia
na na kile nilichokua nimekisoma kutoka katika miaka yangu mingi ya kusoma
Koran; na hapakuwepo na shaka katika ufahamu wangu tena kwamba hatimaye
nimekutana na Mungu wa kweli. Bado nilikuwa nasoma hadi alfajiri ya siku
iliyofuata, na kwa dhati niliyatoa maisha yangu kwa Yesu.
Imani Mpya
Niliendelea Kufanya Kazi Kwenye Biashara za Baba yangu na sikumweleza lolote
juu ya imani yangu mpya. Ukweli ni kwamba alinipeleka Afrika ya Kusini mwaka
1994 ili kunitafutia nafasi zaidi za biashara. Nilipokuwepo kule nilikaa siku tatu
pamoja na familia moja ya Kikristo ya kutoka India. Tulipoachana walinipa msalaba
mdogo ukiwa kwenye mkufu ili nivae shingoni. Msalaba huu mdogo ulisababisha
badiliko kubwa maishani mwangu. Baada ya siku chache zisizofikia juma moja, baba
yangu aliugundua mkufu shingoni mwangu akachukia sana kwa sababu, kulingana
na mila za Kiislamu, ni wanawake tu wanaoruhusiwa kuvaa mikufu kwenye shingo
zao. “Kwanini unavaa mkufu huu?” aling’aka.
Ilikuwa kana kwamba ulimi wangu uliongea wenyewe na si mimi wakati nilipojibu,
“Baba huu sio mkufu huu ni msalaba unamwakilisha Yesu, aliyekufa juu ya msalaba
kama huu kwa ajili yangu, yako na watu wote wa ulimwengu mzima. Nilimpokea
Yesu kama Mungu na Mwokozi wangu, na nakuombea na familia nzima mumpokee
Yesu Kristo.” Kwanza baba yangu alizimia pale pale mtaani tulipokuwa. Alipozinduka
alikuwa amekasirika sana kiasi kwamba hata kuongea ilikuwa shida, alininyooshea
kidole. Kwa sauti kali mithili ya farasi akasema; “kaka yako amebadili dini ni lazima
nimuue leo” Popote alipokuwa akienda baba yangu alizoea kubeba bunduki kwapani
iliyokuwa kwenye mfuko wa ngozi. (Matajiri wengi wa Misri hutembea wamebeba
bunduki). Aliichomoa bunduki yake na kunielekezea. Nilianza kukimbia nikishuka
mitaani na nilipochepuka kwa kukata kona nikasikia risasi ikipita nyuma yangu.
Niliendelea kukimbia ili kusalimisha maisha yangu.
Dada yangu alinifanyia rehema na kukusanya vitu vyangu kutoka katika nyumba
ya wazazi wangu. Yeye pamoja na mama yangu walinipa kiasi cha fedha na
nikaingia ndani ya gari langu na kuanza kuendesha jioni ya tarehe 28 Agosti 1994.
Kwa miezi mitatu nilijitahidi kusafiri kupitia kaskazini mwa Misri, Libya, Chad na
Kameruni. Hatimaye nikatua Kongo. Wakati ule nikaugua malaria. Walinitafutia
daktari Mmisri wa kunipima, akasema hadi asubuhi nitakuwa nimeshakufa,
wakafanya mipango ya kupata jeneza kutoka ubalozi wa Misri ulioko Kongo ili
kunisafirisha kunipeleka nyumbani. Kwa mstuko mkubwa wakaniona nimeamka
kesho yake asubuhi. Nilitoka hospitali baada ya siku tano na nikaanza kuwaambia
watu kila mahali kuhusu kile Yesu alichonitendea.
Maisha nikiwa kama Mfuasi wa Yesu Kristo
Miaka kumi imepita tangu nilipompokea Bwana Yesu kama mwokozi wangu.
Aliniita na kunipa uhusiano wangu binafsi na yeye, kitu ambacho Uislamu hautoi
kamwe. Kamwe sijaacha kulia kwa ajili ya watu wangu Waislamu ambao niliwaacha
nyuma, nikimwomba Mungu awakomboe toka katika giza la Uislamu. Kiasi kikubwa
cha taarifa zisizo sahihi zimekuwa zikishirikisha watu kwa njia ya vyombo vya habari
na tovuti.
Lengo langu ni kuwasaidia watu waone waziwazi ni kwanini watu hawa hufanya
kile wanachokifanya. Sitaki kuwachochea watu wakasirike, ila nataka
kuwahamasisha kuamini– kuamini ili Uislamu uanguke na kuwaachilia mateka wake,
katika jina la Yesu.
Kama Yesu Kristo angekuwa anaishi na sisi leo, angesafiri kwenda nchi za
Kiislamu. Angeingia misikitini na kuhubiri neno la Mungu na ujumbe wa wokovu
sawa na alivyofanya katika Hekalu miaka 2000 iliyopita. Angewatembelea Waislamu
majumbani mwao au angekutana nao kwenye maeneo yao ya kufanyia kazi.
Angewaponya Waislamu ambao ni wagonjwa. Angetangaza msamaha wa Mungu
kwa Waislamu watenda dhambi. Angekabiliana na Waislamu kwa kweli yake, na
angewaeleza kuhusu siri ya mbinguni kwa upendo huruma na uangalifu.
Asingewaogopa, asingefikiri kwamba baadhi yao ni magaidi na wangeweza
kumuua au kumdhuru. Yesu Kristo angewaonyesha Waislamu njia ya kwenda
mbinguni kupitia Yeye mwenyewe.
Bwana Yesu Kristo asingewageuzia Waislamu kisogo. Hii ni changamoto yangu
kwa Kanisa. Kunjueni mikono yenu kwa Waislamu. Waonyesheni ushuhuda wa
Kristo. Waambieni Yesu alikufa kwa ajili yao. Wapeni tumaini kwamba dhambi zao
zitasamehewa. Moyo wangu unamlilia Bwana kwa ajili ya Kanisa la Mashariki ya Kati
liguswe na Roho wa Mungu na kuwafungulia milango Waislamu ili waje kwenye
maarifa ya Kristo.
Mark Gabriel ni mwandishi wa kitabu cha Uislamu na Ugaidi (Islam and
Terrorism-Charisma House) Makala haya yamechukuliwa kutoka katika kitabu
hicho.
Mungu mpendwa ninafahamu kwamba dhambi zangu zimenitenga na wewe, na
nataka kukiri dhambi zangu. NASIKITIKA NIMEKUKOSEA. Ninajua kwamba
unanipenda ulimtoa Yesu afe msalabani badala yangu, akichukua adhabu ya dhambi
zangu. AKSANTE. Sasa hivi nakuomba uingie na kuyatawala maisha yangu.
Ninajitoa nafsi yangu kwako. Tafadhali anza kuyaongoza maisha yangu.
NAKUHITAJI. Aksante kwa kunipa uzima wa milele. Katika jina la Yesu ninaomba.
Amina.
Tunatoa vijarida, vipeperushi, kanda za kaseti na za video za aina mbalimbali
zinazofunua na kuchambua mafundisho yote makubwa ya Uislamu. Taarifa hizi ni za
uhakika kwa kujibu swali lolote unaloweza kuwa nalo kuhusu Uislamu. Saidia
kueneza ukweli. Vitu vyote hivyo utavipata bure kama ukiagiza.
Kwa maelezo zaidi kuhusu ACMTC TANZANIA, au jinsi utakavyoweza
kujihusisha, wasiliana na Meja Frank & Elina Materu: S.L.P. 7579 Dar es
Salaam, Tanzania. Barua pepe: materufrank@yahoo.com
|